Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifaa cha kisasa cha kuchunguza kiharusi chaanza kutumika MOI

Thu, 10 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI)  imeanza kuwafanyia uchunguzi wagonjwa kwa kutumia kifaa cha kidigatili cha kuchukua picha za ndani ya mwili kwa kutumia mionzi (Digital X-Ray) inayotoa majibu papo kwa papo na darubini ya kisasa kwa wagonjwa wa kiharusi.

Mashine hiyo inatoa matokeo ndani ya dakika moja mara baada ya mgonjwa kuchukuliwa vipimo.

Akizungumza leo Jumatano Januari 9, 2019 wakati wa ziara maalum ya Wizara ya Afya kwa taasisi zake, Dk Shaaban Hamisi, ambaye ni bingwa wa magonjwa ya ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, amesema darubini hiyo iliyonunuliwa kwa Sh1 bilioni imewezesha taasisi yake kurahisisha huduma za wagonjwa wenye matatizo ya ubongo, hasa wa kiharusi ambao awali walitegemea matibabu nje ya nchi.

“Mashine hizi ni za kipekee kwa nchi za Afrika Mashariki na zimechangia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa ambao hapo zamani walikwenda nje ya nchi kwa gharama ya dola 60,000 za Kimarekani 60,000 (sawa na zaidi ya milioni 130) na kwa sasa tunatibu mtu mmoja kila siku kwa Sh10 milioni hivyo ni gharama kubwa imeokolewa,” amesema Dk Hamisi.

Bingwa wa kutibu kwa kutumia vipimo vya Tehama, Dk Ngina Mitti amesema kwa sasa ndani ya saa 24, MOI inaokoa fedha nyingi na kutibu wagonjwa wengi kwa siku.

Mgonjwa aliyekuwa akipata matibabu ya mifupa na mishipa, Patricia Luoga ameishauri serikali iajiri wataalamu wengi zaidi wanaoweza kutumia vifaa hiyo vya kisasa ili kuongeza nguvu kwa wataalamu waliopo.



Chanzo: mwananchi.co.tz