Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya, Malawi, Ghana kujaribu chanjo ya malaria

53679 CHANJO+PIC

Tue, 23 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lilongwe, Malawi. Chanjo ya kwanza ya malaria duniani itajaribiwa kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Ghana, Kenya na Malawi kuanzia wiki hii.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema chanjo hizo zinaweza kuokoa maisha ya maelfu wakati huu ambao watu wameendelea kupoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria.

Mpango huo ambao uko katika majaribio utahusisha zaidi ya watoto 700,000 wa umri kati ya miezi mitano na mwaka mmoja na nusu.

Haijathibitika kwamba chanjo hiyo inaweza kufanya kazi kwa asilimia 100, lakini wataalamu wa masuala ya afya wanasema chanjo hiyo ni hatua muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Hii inafuata miongo kadhaa ya tafiti ya kutafuta ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo duniani.

Chanjo hiyo mpya, itakwenda sambamba na hatua nyingine za kujikinga kama vile neti, dawa za kufukuza mbu na dawa za kukinga malaria.

Wakati wa majaribio, maelfu ya watoto watapewa chanjo hiyo mara nne katika kipindi cha miaka miwili.

Aprili 25 ni siku ya maadhimisho ya ugojwa wa malaria duniani , nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, changamoto bado ni kubwa katika kuutokomeza ugonjwa huo kwa kuzingatia  malengo ya WHO ya kumaliza ugojwa huo ifikapo mwaka 2030.

Ripoti ya WHO kwa miaka miwili mfululizo 2015-2016 ilibaini kwamba zaidi ya asilimia arobaini ya raia wa DRC walifariki  dunia kutokana na ugonjwa huo.

Pia kwa mujibu wa ripoti hiyo Congo na Nigeria zimekuwa nchi za kwanza duniani kuathiriwa na ugonjwa huo.



Chanzo: mwananchi.co.tz