Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Waziri Ummy juu ya matumizi ya P2

P2 Wabunge (600 X 357) Kauli ya Waziri Ummy juu ya matumizi ya P2

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusambaa kwa maneno yanayosomeka ‘Amka umeze P2” ikiwa ni saa chache baada ya Valentine’s day kupita, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amejitokeza na kuandika yafuatayo.

“Inaweza kuonekana ni utani lakini huu ndio ukweli hasa kwa baadhi ya Watoto wetu wa kike walio shuleni, P2 ni dawa ya kuzuia mimba zisizotarajiwa mathalani kutokana na kubakwa, kondom kupasuka na kwa waliokosea hesabu za siku zao za hedhi na hivyo kujikuta wamefanya yao na ili kuepuka kutoa mimba (abortion) au kuzaa Watoto wasiowatarajia wanaweza kutumia dawa hii”

"Hivyo kama Serikali tusingependa kuziwekea vikwazo dawa hizi, tunatamani upatikanaji wake usiwe na changamoto yaani ziwe zinapatikana haraka na kwa kila mwenye uhitaji aliepata dharura, hata hivyo tunatambua kwamba kuna mis-use ya hizi dawa hasa kwa Watoto wa Shule ambao kwa sasa inaonekana wanaogopa zaidi mimba kuliko UKIMWI!, matumizi holela ya P2 yanaweza kuzalisha matatizo mengine makubwa ya kiafya kwa wasichana/wanawake"

"Wataalam wetu wamenihakikishia kuwa matumizi holela na ya mara kwa mara ya P2 yanaweza kusababisha ugumba na saratani, tunaendelea kuliangalia suala hili kwa mapana yake, wakati tunaendelea kulijadili ndani ya Serikali na wadau, hatua ya haraka tutakazo kuchukua ni kuongeza kasi ya utoaji elimi ya juu ya madhara ya matumizi holela ya dawa hizi (P2)”

"Nimeshawaelekeza timu yangu kulitekeleza hili haraka, nasi Wazazi/Walezi tusione aibu kuwaeleza mabint zetu madhara ya ngono za mapema na kuepuka ngono zisizo salama, kama Binti/Msichana unaona hupo tayari kuzaa basi unashauriwa kutumia njia za uzazi wa mpango na siyo P2"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live