Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Waziri Dr. Gwajima baada ya Marekani kutoa Tsh. Bilioni 437

Fdhgg Kauli ya Waziri Dr. Gwajima baada ya Marekani kutoa Tsh. Bilioni 437

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima amelishukuru Shirika la Misaada la Watu wa Marekani USAID kwa msaada wa fedha Sh bilioni 437 na chanjo za Janssen 165,000 zilizowasili nchini tarehe 13, Novemba 2021.

Akizungumza na mtendaji mkuu wa shirika hilo leo Novemba 15 jijini Dar es Salaam, Dk Gwajima amesema fedha hizo zitasaidia kutekeleza miradi na kuboresha sekta ya afya.

Aidha, amesema kuwa Serikali ya Marekani imejipanga kuisaidia Tanzania kudhibiti magonjwa yanayoambukiza ikiwemo Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na Uviko 19 ambapo mwaka 2022 zaidi ya Sh 437 zitatolewa kutekeleza miradi ya kijamii katika kipindi cha miaka mitano kwa lengo la kuboresha huduma sekta ya Afya na kuimarisha ustawi na maendeleo ya vijana nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live