Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Kati ya watu 10, watano wana tatizo la kuchakata sukari: (+picha)

2 1 660x400 "Kati ya watu 10, watano wana tatizo la kuchakata sukari: (+picha)

Tue, 17 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Watanzania wametakiwa kujitokeza kupima afya zao mara kwa mara ili kudhibiti madhara ya magonjwa yasiyoambukiza hususani ugonjwa wa kisukari ambao unakadiriwa kuweza kuathiri asilimia 20 ya Watanzania.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Kituo kinachotoa huduma za ugonjwa wa kisukari- St Laurent, Dk. Mary Maige wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani.

Maadhimisho hayo ambayo ambayo hufanyika kila ifikapo Novemba 14, yalienda sambamba na utoaji wa huduma za upimaji na ushauri wa kitabibu bure.

Katika maadhimisho hayo ya mwaka huu yalidhaminiwa na  Kampuni ya Abel & Fernandes Communications pamoja na Quincewood Consulting kupitia miradi yake ya  uwajibikaji kwa jamii.

Kampuni hizo zimeungana na Kituo cha Kisukari St. Laurent katika kuisaidia Serikali katika mapambano dhidi ya Kisukari kwa kujenga uelewa kuhusu ugonjwa huo ambao kwa mujibuwa takwimu za wizara ya afya hadi sasa umeathiri zaidi ya watu milioni 1.5 nchini.

Akizungumzia maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Kituo cha Kisukari- St Laurent, Dk. Mary Maige alisema kauli mbiu ya maadhimisho ya Kisukari duniani  kwa mwaka huu ni “Uuguzi na Kisukari”.

Amesema mwaka 2012 walifanya utafiti nchi nzima na kubaini kati ya watu 10, watu watano wana tatizo la kuchakata sukari mwilini hivyo kubaini kuwa asilimia 20 ya watanzania wana matatizo ya kuchakata kisukari.

“Kwa hiyo hili tatizo linazidi kuongeza, kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele tatizo linaendelea kuongezeka na tunatakiwa kuongeza juhudi zaidi ili kudhibiti tatizo hili ambalo linachangiwa kwa kiasi kikubwa na mtindo wetu wa maisha,”  Dk. Mary

Aidha,  Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Abel & Fernandes, Fatma Fernandes alisema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kwa pamoja wanaungana na wauguzi kuzuia na kutoa muongozo kuhusu Kisukari.

“Pia tunatoa huduma kwa mamia ya jamii kwa malengo ya kuwapatia taarifa muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari na namna ya kukabiliana nao” Fatma Fernandes

“Maadhimisho ya mwaka huu ni muhimu kwetu wote kwani yanatoa fursa ya kupata huduma za afya bure kwa malengo ya kuboresha afya za watanzania wanaoishi na Kisukari, pia kuboresha maisha ya watu wanaoishi na ugonjwa huo,” Fatma Fernandes

Naye Katibu Mwenezi wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Johari Yusufu alisema kampeni hiyo ya mwaka huu inalenga kuwapa motisha wauguzi kutekeleza majukumu yao kwa uweledi ili kuwapatia huduma bora, stahiki na zenye staha wagonjwa wa kisukari nchini.

Alisema wauguzi wanahesabika kuwa nusu ya wafanyakazi wote wa sekta ya afya nchini. Ni kada mojawapo inayoweza kuwapatia huduma bora watu wanaoishi na magonjwa mbalimbali. Watu wanaoishi na Kisukari huhitaji zaidi msaada wa wauguzi katika kutibu tatizo hilo.

“Kwa hiyo tunawashauri wananchi wawe wanakwenda hospitali kucheki afya zao mara kwa mara,” amesema.

Chanzo: millardayo.com