Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kata ya Kitangiri kujengewa Zahanati

B3576fe619e47a0408127c8211b7f34f Kata ya Kitangiri kujengewa Zahanati

Thu, 22 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ilemela kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM),Dk Angelina Mabula amewahidi wakazi wa kata ya Kitangiri kuwa atajenga zahanati katika kata hiyo.

Ahadi hiyo aliitoa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Kitangiri sokoni. Dk Mabula aliahidi pia kuboresha miundo mbinu ya soko ya Kitangiri.

Dk Mabula alisema tayari Serikali ya CCM imetenga milioni 300 kwajili ya ujenzi wa mwalo wa Mihama uliopo katika kata hiyo.Aliahidi kuhakikisha atajenga barabara za Jiwe kuu kuelekea Mihama katika kiwango cha lami na tayari milioni 67/- zimetengwa kwajili ya ujenzi huo.

Katika sekta ya Elimu,Dk Mabula alisema katika wilaya ya Ilemela wamefanikiwa kujenga madarasa 69 kwa shule za msingi na madarasa 54 katika shule za sekondari za wilaya yao. Alisema tayari wametenga milioni 39 kwajili ya kujenga madarasa matatu katika shule ya sekondari ya Mwinuko na milioni 30 kwajili ya kujenga maabara katika shule hiyo.

Alisema wametenga pia milioni 10 kwajili ya kujenga nyumba ya katika shule ya sekondari Mihama. Mgombea udiwani wa kata ya Kitangiri kupita CCM,Donald Ndaro alisema atashirikiana na Dk Mabula katika kuhakikisha wanajenga zahanati katika kata yao.

Meneja kampeni wa Dk Angelina, Kazungu Safari aliwaomba wakazi wa kata ya Kitangiri wahakikishe wanawahi mapema siku ya kupigia kura na kuchagua wagombea wa CCM.

Chanzo: habarileo.co.tz