Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kasulu kujenga hospitali ya wilaya kwa Sh1.5 bilioni

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Halmashauri ya Wilaya ya Kasul mkoani Kigoma inatarajia kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya itakayogharimu Sh1.5 bilioni.

Kaimu mganga mkuu (DMO) wa halmashauri hiyo, Dk Kawamba Kawambwa ametoa taarifa hiyo kwa timu ya wilaya iliyotembelea eneo la ujenzi wa mradi huo.

Hospitali hiyo itajengwa katika kijiji cha Nyamnyusi ambako wananchi wamekubali kutoa eneo itakapojengwa.

Dk Kawambwa amesema ujenzi huo utakamilika Juni mwakani ukihusisha jengo la utawala, wodi, maabara, famasia na huduma kwa wagonjwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kasulu, Yohana Mshita amesema hospitali hiyo itakapojengwa itapunguza kero wanazopata wagonjwa kufuata huduma mbali na makazi yao.

"Hospitali hii itasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya muda ya wilaya iliyopo Mlimani, hivyo kusogeza huduma za afya karibu na wananchi," amesema Mshita.

Baadhi ya wakazi wa Nyamnyusi wamesema wametoa ardhi yao kwa ajili ya kusaidia upatikanaji huduma ya afya karibu na makazi yao.

Daniel Ruyagaza amesema Serikali haina budi kuboresha zahanati na vituo vya afya ili viendelee kutoa huduma bora ya afya.

Halmashauri hiyo ina zahanati 32 na vituo vitano vya afya, haina hospitali ya wilaya jambo linalofanya wagonjwa kwenda kutibiwa hospitali za halmashauri nyingine wanapopewa rufaa.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz