Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kasi ya maambukizi ya Corona yaongezeka Ulaya

GERMN.jfif Kasi ya maambukizi ya Corona yaongezeka Ulaya

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani WHO, limetoa tahadhari ya kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini Ujerumani huku ikibainisha kuwa jumla ya watu 500,000 wanakadiriwa kupoteza maisha barani Ulaya pindi wimbi lingine litakapoinuka.

Taarifa hii imetolewa wakati Uingereza ikiwa imeidhinisha matumizi ya dawa za vidonge zitakaotumika kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Kuzidi kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo kumepelekea Shirika hilo kupitia kwa mkurugenzi wa kitengo cha dharura, Michael Ryan, kutoa tahadhari hiyo'

"Nafikiri hii ni hatua ya hatari zaidi kwa Ulaya, na inafikirisha kwani dunia yote inafahamu dhahiri kuwa kuna chanjo za kutosha lakini bado hali si shwari". Amesema Mkurugenzi huyo.

Ujerumani imevunja rekodi kwa kuwa na wagonjwa wapya wapatao 34,000 ndani ya masaa 24 wakifuatiwa na Croatia wenye jumla ya maambukizi 6,310.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live