Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kasi ya kuchanja imepungua kidogo - Rais Samia

Samia Kia.png Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Wed, 4 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Uviko - 19 ikiwa ni pamoja na kuendelea kuchanja.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Mei 03/2022 aliposhiriki Baraza la Eid katika ukumbi wa J. K Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa pamoja na takwimu kuonyesha kuwa ugonjwa huo unapungua nchini lakini ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari ili kujikinga zaidi.

"Katika masafari yangu nilifanya mazungumzo na watu kadhaa, nilishangazwa na mmoja kati yao, ananiambia unajua kirusi kijacho kitakuwa kikali kuliko hiki, nikamuuliza umejuaje?, ni sayansi au ni cha Mungu na kama ni cha Mungu umejuaje, na kama ni sayansi kwanini mnavitengeneza, ombi langu ni kuendelea kuchukua hadhari katika kujikinga"

 

Aidha Rais Samia ameeleza kuwa ni kweli kasi ya kuchanja imepungua lakini serikali inajiandaa kuja na kampeni mpya ya kuongeza kasi ya watu kuchanja, huku akisema asilimia 13 ndio waliochanja hadi sasa

"Kwa sasa hivi tumeweza kuchanja watu 3,950839 sawa na asilimia 13 ya kundi tulilokusudia kulichanja, ukiangalia takwimu hizi sisi tupo mbele kidogo kuliko hata wenzetu walioanza kabla ya sisi na tunaahidi kwamba tutaongeza jitihada katika kufanikisha watu kuchanja" amesema Rais Samia

 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live