Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapufi ataka serikali ikamilishe ujenzi Hospitali ya Katavi

WhatsApp Image 2021 05 11 At 12.48.07.jpeg Kapufi ataka serikali ikamilishe ujenzi Hospitali ya Katavi

Tue, 11 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akiuliza swali bungeni leo, amesema katika ziara ya Hayati John Magufuli Katavi, aliyekuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliwahakikishia kuwa ifikapo Julai, 2020 ujenzi wake utakuwa umekamilika.

“Serikali inasema nini kwa wananchi wa Katavi kutokana na ahadi hizi zisizotekelezeka, umbali kutokea Katavi ikitokea kuna mgonjwa anahitaji tiba ya madaktari bingwa, au umpeleke Mbeya, Mwanza au Dar es salaam, ukiwa katika hali ya mahututi umbali huu ni mrefu zaidi, serikali inasemaje katika kuwanusuru wananchi kuja na suala la dharura ikizingatiwa kuna hospitali zimejengwa kwa zaidi ya hiyo Sh.Bilioni 9,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Godwin Mollel, amesema kiasi cha Sh. bilioni 5.85 zitatumika kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo ifikapo Januari 2022 ambapo mradi huo unagharimu Sh. bilioni 9.82.

Dk.Mollel amesema Sh.milioni 250 kwa mwaka zinatumika kwa ajili ya gari la wagonjwa kupeleka wagonjwa wa rufaa kwenye hospitali za rufaa.

Chanzo: ippmedia.com