Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampeni ya usafi wa kudunia yazinduliwa

16685 Pic+usafi TanzaniaWeb

Tue, 11 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Licha ya kuanzishwa kwa kampeni mbalimbali za usafi katika baadhi ya maeneo, kampeni hizo bado hazijaweza kuleta mabadiliko endelevu kutokana na wananchi kukosa uelewa wa kutosha juu ya kampeni hizo.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Septemba 10, 2018, na Mratibu wa Shirika la kijamii linalojihusisha na uhamasishaji wa usafi wa Jiji Nipe Fagio, Navonaeli Kaniki wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya usafi ya Let'do it ya kidunia iliyozinduliwa jijini hapa.

Amesema wananchi wanatakiwa kupewa elimu itakayowajengea uwezo wa kutambua madhara yatokanayo na taka.

"Tutakachofanya sasa ni kuanzisha mijadala mbalimbali kwa kutumia makundi ya watu ambao tumewaandaa kuhamasisha na kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu usafi wa mazingira," amesema Kaniki.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuondoa taka kutoka kwenye mazingira asili na kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa usafi katika maeneo yao.

Aidha kampeni hiyo inazinduliwa zikiwa zimebaki siku nne kuadhimisha siku ya usafi duniani ambapo Tanzania itaungana na nchi nyingine 150 kuadhimisha siku hiyo inayofanyika Septemba 15 kila mwaka.

"Lengo la siku ya usafi duniani ni kuongeza uelewa wa madhara ya tatizo la taka na uchafuzi wa mazingira unaotokana na plastiki hapa nchini na duniani," amesema.

Kwa upande wake, mjasiriamali na mdau wa usafi wa mazingira, Fortunatus Ekklesiah amesema tatizo lililopo kwa wananchi linatokana na upofu walionao.

"Unakuta mtu anaziona taka zimezagaa katika eneo lake hawezi kuzitoa na kuzitupa katika eneo sahihi," amesema.

Amesema asilimia kubwa ya taka zinazochafua mazingira ni plastiki na kuongeza kuwa endapo hazitadhibitiwa si tu zinachafua mazingira bali kuathiri afya za wananchi.

Chanzo: mwananchi.co.tz