Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampeni ya 'pedi bila kodi' yapamba moto Twitter

63723 Pic+taulo

Fri, 21 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Baada ya Serikali ya Tanzania  kupendekeza kurejesha Kodi ya Ongezeko la Thamani  (VAT) kwenye taulo za kike katika bajeti ijayo ya mwaka 2019/20, kampeni ya ‘pedi bila kodi’ imeanza kupamba moto kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter.

Wanaharakati mbalimbali wameamua kufanya kampeni hiyo kuishinikiza Serikali iondoe kodi kwenye taulo za kike wakidai suala la hedhi sio chaguo wala starehe ni maumbile ya kibaiolojia.

Katika bajeti ya mwaka 2018/2019, Serikali iliondoa VAT kwenye taulo za kike lakini bajeti ya 2019/2020 imerejesha kodi hiyo kwa madai ya walengwa kutonufaika.

Walengwa wa punguzo hilo walikuwa wanafunzi wa kike ambao tafiti mbalimbali zilionyesha kila mwezi hushindwa kwenda shuleni kati ya siku tatu mpaka nne kutokana na ukosefu wa bedi.

Mrembo wa Tanzania mwaka 2005, Nancy Sumari kupitia ukurasa wale wa Instagram ameandika kwa ajili ya mama na mabinti zetu na wanawake wenzetu wote, na iwe pedi bila kodi.

Hii ni hashtag anayoitumia kila anapoposti kitu ikiwa ni uhamasishaji wa kuondolewa kodi kwenye taulo za kike.

Pia Soma

Pam Kiambi katika ukurasa wake wa Twitter amesema wakati wa hedhi sio  starehe hivyo Serikali inapaswa kuwekea wanafunzi wa kike shuleni mazingira ya kupata taulo hizo kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake, Christina Chacha kwenye ukurasa wake wa Twiter ameandika wanawake na wasichana wahakikishiwe pedi kwa bei ya kawaida na wanayoweza kumudu bila kulipiwa kodi.

Naye Petrida Paul kwenye ukurasa wake wa Twiter pia ameandika anaunga mkono kampeni hiyo akiwaangalia zaidi wanawake na wasichana wa vijijini kuwekewa gharama ndogo watakayoweza kumudu.

Pia  Priya Nikole ameunga mkono kampeni hiyo akisema kitendo cha  kuingia kwenye hedhi kila mwezi sio chaguo la mwanamke ni suala la maumbile hivyo vifaa vya kujikinga vinapaswa kufikiwa kwa bei naafuu wanayoweza kumudu.

Naye Halima Lila ameiomba Serikali kutizama upya suala hilo akidai kuwa wanawake na wasichana hawana chaguo hivyo, wanafunzi wa kike waandaliwe mazingira ya kufata vifaa vya kujikinga na hedhi bila kodi.

Chanzo: mwananchi.co.tz