Samaia amesema hayo leo Iluku jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kuawaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni.
“Ninakusudia kuunda kamati ya wataalamu waliangalie suala la corona kwa upana wake halafu watushauri serikali, watupe upeo wa tatizo hili lilivyo na hayo yanayopendekezwa na ulimwengu je yakoje," amesema Samia.
"Hatuwezi kujitenga kama kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kufanya utafiti wa kwetu,”
Kuhusu suala la bima ya afya amemtaka waziri wa afya kuhakikisha bima za afya zinakuwa na uwezo wa kununua dawa kwa wagonjwa. Pia amesema kuwa bohari ya dawa (MSD) inatakiwa kuongeza upatikanaji wa dawa za kutosha katika hospitali na zahanati.