Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kama siyo Mkapa, bima ya afya ingelikuwa ndoto

C48bdb148408da99132a6ead0f04e335 Kama siyo Mkapa, bima ya afya ingelikuwa ndoto

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMA kuna ujasiri ulifanyika katika siasa na kufaidisha Tanzania ya sasa pamoja na upinzani mkubwa wa kuwepo kwake, ni uamuzi wa kutekeleza safari ya kuanzishwa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kusaidia kuimarisha sekta ya afya nchini.

Uamuzi huo wa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa wa kuwa na NHIF pamoja na upinzani na vikwazo kutoka ndani na nje umewezesha Watanzania wengi leo kuwa na sauti ya kutaka kufikiwa na bima ya afya, hasa taifa hili linapoanza safari ya kutafuta uchumi wa kati wa juu.

Ingawa kuondoka kwake duniani na kuzikwa kunaacha simanzi kubwa miongoni mwa viongozi wakubwa wa nchi, Watanzania kwa ujumla na katika nyanja za kimataifa, faraja kubwa inaonekana ya kuenzi uhai wa Rais Mkapa hasa kutokana na kufanikisha uwapo wa bima ya taifa ya afya ambayo ina historia ndefu.

Pamoja na mambo makubwa ambayo Rais Mkapa aliyafanya enzi za uhai wake lakini kuna upekee wa kutosha kuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, si tu kwa kuasisi bali kuusimamia mpaka ukatulia katika kipindi cha mawimbi mazito kutoka katika Chama cha Walimu (CWT) kilichoongoza katika kupinga bima hiyo huku watumishi nao wakiwa hawaelewi.

CWT ilishutumu serikali kwa kuwageuza wao kuwa chombo cha majaribio.

Na walikwenda mbali zaidi kiasi cha kutaka wanachama wao kuacha kujaza fomu za kujiunga na NHIF huku wakisema ni kinyume na katiba ya nchi kukatwa fedha za mshahara bila kuridhia.

Na mbaya zaidi, sio chama hicho tu bali vyama vingine vya wafanyakazi navyo vilipinga vikitaka warejeshewe fedha na watoa huduma.

Hali mbaya ya uhusiano kati ya serikali na waajiriwa wake kuhusu suala la bima ya afya, lilitishia hata uwepo wa NHIF na wafanyakazi wake. Rais Mkapa akiwa muasisi wa mfuko huu alisema hakuna kurudi nyuma, kasoro zirekebishwe na utaratibu uendelee.

Kukiwa na sintofahamu kubwa kwa watumishi wa umma juu ya huduma zitakazotolewa na NHIF, Rais Mkapa alisimama na kuzungumza kupitia maadhimisho ya Wafanyakazi Duniani ya mwaka 2002 mkoani Arusha na kusema, “Changamoto za NHIF ni matokeo ya kutekeleza uamuzi sahihi kwa sababu nzuri.”

Kauli hii ilikuwa na uzito mkubwa sana wa kuifanya NHIF isimame na kuendelea lakini pia hakusita kuitaka NHIF ihakikishe inashughulikia matatizo yanayolet Kama siyo Mkapa, bima ya afya ingelikuwa ndoto watekelezaji wa mpango huo na pia ushauri wa watu wa afya wa Uingereza kuhusu namna ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa uliopanga kuleta mapinduzi ya matibabu nchini Tanzania, ikiwa ni zaidi ya miaka 40 ya suala la afya kuwa la serikali.

Ingawa kwenye miaka ya 1962 Israel ilifanya utafiti na kutoa ushauri wa namna ya kuendesha tiba nchini Tanzania, Serikali ya awamu ya kwanza, kutokana na mazingira ya wakati huo iliona haina sababu ya kutaka watu wake wachangie, kwenye miaka ya 1990 ilionekana dhahiri kwamba lazima kutengenezwe mfumo utakaosaidia wananchi walio wengi kupata huduma za afya huku serikali ikiendelea kupunguziwa mzigo.

Ukisoma kitabu cha ‘A Historical Development of the National Health Insurance Fund of Tanzania – From Resistance to Radiance’ cha mwaka 2011 kilichohaririwa na Profesa Lucian Msambichaka na mwenzake Emmanuel Humba, timu ya ufundi ilitakiwa kuwasilisha hoja za utatuzi na nyongeza zake kabla ya tarehe 31 Januari mwaka 1995.

Timu hiyo ilifanya kazi kubwa ya kuondoa hofu lakini pia mapendekezo yake mengi yalionekana kufaa na mengine mengi pia yalionekana hayataweza kufaa kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania katika masuala yanayohusu tiba na utabibu.

Wakati fulani nilifanya mahojiano na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kwanza wa NHIF baada ya yote kupita, Em manuel Humba kwenye miaka hiyo ya 1990 juu ya kwanini hasa tuwe na NHIF na yeye alikuwa na majibu mengi lakini makubwa zaidi yalikuwa manne.

Humba aliniambia pamoja na kwamba bajeti ya sekta ya afya hasa katika tiba imekuwa ikizidi kupungua na hivyo kuwepo na udhaifu katika kusimamia tiba, ilionesha kwamba kunahitaji udhibiti mkubwa na kianzio ni wafanyakazi na pia utaratibu wa kurejesha fedha za matibabu haufai kwa kuwa unahitaji udhibiti wa hali ya juu.

Mapitio mengi yalifanyika na moja na ulipaji wa ada katika huduma za hospitali za mkoa na wilaya iliyoidhinishwa mwaka 1993 na kuanza kufanyiwa kazi mwaka 1994 ilitoa mwelekeo wa nini kinastahili kufanyika ili kupunguza nakisi ya fedha za huduma.

Mafanikio makubwa katika jimbo la Igunga mkoani Tabora kuhusu mfumo wa bima ya afya ya jamii (CHF) iliwezesha pia kuona kwamba hali hiyo inawezekana kitaifa baada ya kuona aina ya mfumo.

Igunga ambao walianza CHF mwaka 1996 kwa muda huo walionesha kwamba Bima ilikuwa na nafasi ya kubadilisha maisha ya watanzania katika eneo la tiba.

Kulikuwa na shida nyingi ya namna ya kuanzisha mfumo wa taifa wa bima ya afya, na ingawa mchakato wa kuanzishwa kwa bima ulianza mwaka 1992 haikuwezekana mpaka mwaka 1994 wakati baraza la mawaziri lilipoiridhia azimio la uanzishwaji wake na mwaka 2001 ilipoanzishwa rasmi baada ya kupitishwa kwa sheria na kuzingatia matakwa ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwa na mfuko huo, ilani ya 2000-2005.

Sasa tukiwa tunafaidi huduma za NHIF, ni dhahiri Watanzania wanajivunia uamuzi sahihi ya Rais Mkapa na tuna kila sababu za kuhakikisha mfuko huu unalindwa na hasa mafanikio ambayo yamefikiwa.

Ni muhimu watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa huku tukitambua kuwa bado kuna kundi kubwa la watanzania wanaohitaji huduma za bima ya afya hasa vijijini.

Rais Mkapa siku zote alikuwa anataka Watanzania wathubutu kufanya mambo yanayolenga kuboresha maisha yao na ndio maana alisisitiza kuanzisha safari ya Bima ya Afya kwa Watanzania wote. wa na watumishi kupitia vyama vya wafanyakazi na wadau wengine.

Akizungumza mwaka 2012 alipopata fursa ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko katika Ofisi za Kurasini Bendera Tatu alisema:

“Wakati tunaanza tulijua kuwa zingekuwepo changamoto kubwa, lakini tuliazimia kuwa katika suala hili hakuna kurudi nyuma. Huo ndio utamaduni ambao Watanzania tunapaswa kuuendeleza.”

Alisisitiza kuwa ni lazima Watanzania wachangie wenyewe maendeleo na kuboresha afya zao kwa sababu fimbo ya mnyonge ni umoja na mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe ambao muhimili wake mkuu ni afya bora.

Kuna safari ndefu sana ya kuipata hii bima ya afya ambayo kwa sasa inawezesha maelfu kutibiwa hata wanapokuwa hawana uwezo na pia kuwezesha hospitali kutekeleza wajibu wao.

Mchakato na changamoto zake huwezi kuzikisia kwa mtu ambaye hukuwepo. Sisi wengine tulikuwepo, tulishiriki na kuona.

Kiukweli mwaka 1995 serikali iliomba msaada wa kiufundi toka kwa Serikali ya Uingereza kusaidia kupitia upya mapendekezo ya awali ya uwezekano wa kuanzishwa mfumo wa lazima wa bima ya afya kwa wafanyakazi kama ilivyokubaliwa katika kikao cha baraza la mawaziri.

Washauri katika suala hilo walitakiwa kuangalia kwa makini shaka za wadau waandamizi wa mpango huo ambao wakati huo alikuwa Waziri wa Afya, Zakhia Meghji, katibu mkuu wa wizara hiyo wa wakati huo, mganga mkuu (CMO) na wafanyakazi waandamizi wa wizara ya afya.

Aidha walitakiwa pia kuangalia ushauri wa Benki ya Dunia, watekelezaji wa mpango huo na pia ushauri wa watu wa afya wa Uingereza kuhusu namna ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa uliopanga kuleta mapinduzi ya matibabu nchini Tanzania, ikiwa ni zaidi ya miaka 40 ya suala la afya kuwa la serikali.

Ingawa kwenye miaka ya 1962 Israel ilifanya utafiti na kutoa ushauri wa namna ya kuendesha tiba nchini Tanzania, Serikali ya awamu ya kwanza, kutokana na mazingira ya wakati huo iliona haina sababu ya kutaka watu wake wachangie, kwenye miaka ya 1990 ilionekana dhahiri kwamba lazima kutengenezwe mfumo utakaosaidia wananchi walio wengi kupata huduma za afya huku serikali ikiendelea kupunguziwa mzigo.

Ukisoma kitabu cha ‘A Historical Development of the National Health Insurance Fund of Tanzania – From Resistance to Radiance’ cha mwaka 2011 kilichohaririwa na Profesa Lucian Msambichaka na mwenzake Emmanuel Humba, timu ya ufundi ilitakiwa kuwasilisha hoja za utatuzi na nyongeza zake kabla ya tarehe 31 Januari mwaka 1995.

Timu hiyo ilifanya kazi kubwa ya kuondoa hofu lakini pia mapendekezo yake mengi yalionekana kufaa na mengine mengi pia yalionekana hayataweza kufaa kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania katika masuala yanayohusu tiba na utabibu.

Wakati fulani nilifanya mahojiano na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kwanza wa NHIF baada ya yote kupita, Emmanuel Humba kwenye miaka hiyo ya 1990 juu ya kwanini hasa tuwe na NHIF na yeye alikuwa na majibu mengi lakini makubwa zaidi yalikuwa manne.

Humba aliniambia pamoja na kwamba bajeti ya sekta ya afya hasa katika tiba imekuwa ikizidi kupungua na hivyo kuwepo na udhaifu katika kusimamia tiba, ilionesha kwamba kunahitaji udhibiti mkubwa na kianzio ni wafanyakazi na pia utaratibu wa kurejesha fedha za matibabu haufai kwa kuwa unahitaji udhibiti wa hali ya juu.

Mapitio mengi yalifanyika na moja na ulipaji wa ada katika huduma za hospitali za mkoa na wilaya iliyoidhinishwa mwaka 1993 na kuanza kufanyiwa kazi mwaka 1994 ilitoa mwelekeo wa nini kinastahili kufanyika ili kupunguza nakisi ya fedha za huduma.

Mafanikio makubwa katika jimbo la Igunga mkoani Tabora kuhusu mfumo wa bima ya afya ya jamii (CHF) iliwezesha pia kuona kwamba hali hiyo inawezekana kitaifa baada ya kuona aina ya mfumo.

Igunga ambao walianza CHF mwaka 1996 kwa muda huo walionesha kwamba Bima ilikuwa na nafasi ya kubadilisha maisha ya watanzania katika eneo la tiba.

Kulikuwa na shida nyingi ya namna ya kuanzisha mfumo wa taifa wa bima ya afya, na ingawa mchakato wa kuanzishwa kwa bima ulianza mwaka 1992 haikuwezekana mpaka mwaka 1994 wakati baraza la mawaziri lilipoiridhia azimio la uanzishwaji wake na mwaka 2001 ilipoanzishwa rasmi baada ya kupitishwa kwa sheria na kuzingatia matakwa ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwa na mfuko huo, ilani ya 2000-2005.

Sasa tukiwa tunafaidi huduma za NHIF, ni dhahiri Watanzania wanajivunia uamuzi sahihi ya Rais Mkapa na tuna kila sababu za kuhakikisha mfuko huu unalindwa na hasa mafanikio ambayo yamefikiwa.

Ni muhimu watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa huku tukitambua kuwa bado kuna kundi kubwa la watanzania wanaohitaji huduma za bima ya afya hasa vijijini.

Rais Mkapa siku zote alikuwa anataka Watanzania wathubutu kufanya mambo yanayolenga kuboresha maisha yao na ndio maana alisisitiza kuanzisha safari ya Bima ya Afya kwa Watanzania wote.

Chanzo: habarileo.co.tz