Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KUKU ALIYETOLEWA KWA MJAMZITO APELEKWA MAABARA KWA UCHUMGUZI

Capture 537?fit=727%2C429 KUKU ALIYETOLEWA KWA MJAMZITO APELEKWA MAABARA KWA UCHUMGUZI

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Uvinza mkoani Kigoma, amekutwa na kuku kwenye kizazi baada ya kufika katika kituo cha afya cha Uvinza, akilalamika kuwa anaumwa tumbo na katika uchunguzi daktari akabaini uwepo wa kifaranga hicho ambacho walifanikiwa kukitoa.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Simon Chacha, uchunguzi wa awali, tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina au ukatili kwa maana ya kuku huyo kuingizwa.

Hakuwa na ujauzito alifika hospitali akadai anaumwa tumbo baada ya uchunguzi madaktari wakaona kifaranga cha Kuku kwenye kizazi na tayari wamekitoa, tukio hilo limefanyika nadhani kwa imani za kishirikina”, amesema Dkt. Simon.

Dkt. Ameongeza kuwa “Nimeagiza afanyiwe upasuaji ili kujihakikishia zaidi nini kimetokea ila kwa kufanyiwa kitendo hicho tayari ameharibiwa kizazi”.

Jeshi la polisi Mkoa wa Kigoma limesema kuwa kuku aliyekutwa kwenye kizazi cha mwanamke mkoani humo, atapelekwa kwenye Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya kuchunguzwa kwani si kawaida kwa binadamu kujifungua kiumbe cha namna ile.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma James Manyama, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, na kusema kuwa tukio la mwanamke huyo kujifungua kuku lilitokea siku ya Desemba 5, 2020, katika kituo cha afya Uvinza.

“Kwa kuwa tukio hili siyo la kawaida kwenye jamii, jeshi la polisi tutachukua kiumbe hicho kwa ajili ya kupeleka Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi kwani siyo kawaida kwa binadamu kujifungua kuku”, amesema Kamanda Manyama.

Chanzo: zanzibar24.co.tz