Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi kukatisha dawa kunavyoongeza magonjwa ya akili na madhara mengine

Dsfs Jinsi kukatisha dawa kunavyoongeza magonjwa ya akili na madhara mengine

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: Nipashe

MOJA ya shida kubwa katika magonjwa ya akili, ni mtu kupata hali tofauti ya uhalisia, mabadiliko ya kufikiri, kuhisi na kutenda.

Mabadiliko hayo yanapojitokeza yanaweza kumfanya mhusika mwenye shida ya akili, anaweza kuharibu vitu na kuwajeruhi, hata kudiriki madhara ya kupoteza maisha ya wanaomzunguka.

Mtu anapokuwa katika hali hiyo anakuwa tofauti hali inayoweza kumfanya alete madhara, pasipo kujua hatari iliyoko.

Wapo waliochoma moto nyumba na wanapodadisiwa kulikoni hatua hiyo, hisia zinaangukia tafsiri tofauti kuhusu mali au nafsi ya mhusika, hata binafsi akidhani anajitetea dhidi ya mabaya yasiyokuwapo.

Hapo ndio kuna sababu za wagonjwa wengi wa akili kupelekwa vituo vya polisi, kupata kesi za jinai mfano kesi za mauaji kwa matendo kama hayo.

Matukio mengi ya kihalifu, mara nyingine yanahusisha watu ambao wamepata shida za akili, kukiwapo vyanzo mbalimbali, mathalan wapo ambao wametumia dawa za kulevya.

Ni aina ya watu katika fikra hizo potofu zitokanazo na athari tajwa, katika harakati za kukabiliana na kiu ya dawa ya kulevya (alosto) wanathibitika kupora, hata kufikia ngazi wanabomoa nyumba ili wapate fedha au vitu vya kuuza kukidhi mahitaji yao.

Kunapofanyika hilo, huwa kunawaacha wanaangukia kwenye mikono ya sheria kutumikia kesi za jinai.

Hali kadhalika, wapo wanaovunja sheria hali ya kuchanganyikiwa inapojitokeza ghafla au katika dalili za awali. Kwa wanaoanza ghafla, kuna kundi la wenye matatizo ya kifafa chenye kuchanganyikiwa.

Mtu anazirai na kisha anapozinduka kutoka kwenye degedege, huwa anaambatana na mabadiliko ya tabia.

Kuchanganyikiwa kunakoendana na balaa la kuchukua hatua zenye matukio ya hatari, baadhi wanabeba vifaa hatari na kupiga wengine au anajijeruhi.

DALILI ZA AWALI

Kuna dalili za awali zinazojitokeza na kutajwa kwa mwenye mwelekeo wa shida ya akili. Dalili za awali za jumla huwa anakosa usingizi, hasira zilizopitiliza, anazungumza visivyoeleweka, vipindi vya huzuni zilizopitiliza, kuzubaa, msahaulifu wa kuzungumza au kucheka bila ya sababu.

Ujumla wake kitaalamu, zinatoa ishara ya dalili za shida ya akili inayoendelea. Ni bahati mbaya wengi si wanaochukua hatua kuwahi matibabu, hivyo wanamuacha mtu anaendelea kuugua akili hadi anapopata mabadiliko ngazi ya tabia hatarishi.

Mfano hai, kuna suala la mtu kumpiga au kujeruhi mwenzake, huwa kuna nyakati hali hizo zinaweza kumfanya akaharibu vitu, kujeruhi mtu au hata kumuua.

Matatizo hayo yanapojitokeza yana athari kufikia mkono wa sheria, maana unatoa nafasi ya kusikiliza upande wa pili waliopoteza ndugu zao au kuharibiwa vifaa.

Kuna kundi la tatu; wanaoanza matibabu ya akili, ila wameyaacha kwa sababu mbalimbali kama vile za kifedha, kuhisi wamepona, ushawishi wa ndugu kutafuta tiba mbadala au maudhi ya dawa.

Matibabu ya akili huchukua muda mrefu na hili linawafanya wengine wasiwe na ufuasi mzuri wa dawa hasa wanapohisi wamepona.

Hali ya ugonjwa hujirudia pindi mtu anapoacha dawa ya bila maelekezo sahihi kutoka kwa daktari. Hali inaporudia, huja na dalili za awali, ikiwamo tabia zenye madhara kama yaliyotajwa.

TABIA HATARI

Mtu huenda asijue ni wakati gani anapatwa na hali hiyo, hata akatenda kinyume na sheria. Yapo matukio ya kujiua, baadhi yakihusianishwa na shida ya akili. Wapo wa makundi ya wagonjwa yenye majina ya kitaalamu: Sonona, kundi linaloongoza kujiua; wagonjwa wa Baipola; na Sikizofrenia.

Mwenye sonona hupitia vipindi vya huzuni, upweke, hatia na kujiona hana thamani kabisa, sasa akishikwa na mawazo ya kukatisha maisha.

Hali hiyo inapozidi wiki mbili au zaidi pasipo matibabu kuwapo hatua za kitabibu, kujiua kunakuwapo karibu sana.

Wagonjwa kutoka makundi ya Baipola na Sikizofrenia, kuna wakati wanajihisi wanasikia sauti ambazo kiuhalisia hazipo na zinaweza kambatana na kutoa maelekezo ya mtu ajiue.

Hapo ndipo hatari yake inachukua nafasi mtu mtu akiitikia hilo anajiua, ingawa mawazo yake nayo yakamtuma upande wa pili, anaweza kufanya matendo ya mauaji kwa wengine.

Ni hali ya kubadili uhalisia na akili ikiamini inachokifikiri ni moja ya matukio ambayo yapo naye katika kuichukulia hatua anangukia kudhuru kabisa.

Kwa mama anayetoka kujifungua na akachanganyikiwa akili, ana hatari ya kumdhuru mtoto endapo atamwona kwa tafsiri tofauti na uhalisia wa jamii.

Wapo wanaojikuta hata wakadhuru mtoto akimfananisha ameshika nyoka. Wakati mwingine mtu mwenye changamoto ya akili, anaweza kusikia sauti zinazomwamrisha kutenda matendo ya kuharibu au kudhuru wanaomzunguka akitawaliwa na hisia ni adui zake.

UMUHIMU WA TIBA

Kunatajwa kuna umuhimu wa tiba ya awali, kwa mtu ambaye ameshaanza kupata dalili za magonjwa ya akili ambayo katika sura moja inayosaidia madhara kutoka kwa wahusika.

Jamii inapochangia kuwezesha kundi hilo kuwa na hitaji la msaada, ni mchango katika kupunguza idadi ya wagonjwa wa akili hata katikia mikono ya jinai kisheria.

Chanzo: Nipashe