Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi Watu wenye vitambi walivyo katika hatari ya kupata saratani

1401 Kitambi

Wed, 17 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo January 16, 2018, Nikusogezee utafiti uliofanywa ambao umeonesha kuwa unene unaweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani, hasa kwa mafuta yaliyoko tumboni yanaleta hatari kubwa zaidi. Utafiti mpya umeonesha kuwa mafuta yaliyoko tumboni yanaweza kuzalisha protini inayohamasisha seli za kawaida kuwa seli za saratani.

Unene umethibitishwa kuhusika na saratani za aina mbalimbali Duniani kama saratani ya matiti na utumbo mpana. Watafiti wa chuo kikuu cha Michigan cha Marekani wamesema, katika upande wa tathmini ya saratani, kuangalia kiwango cha mafuta tumboni ni sahihi zaidi ikilinganishwa na kutathmini hali ya unene wa mwili.

Timu hiyo ya watafiti imetoa ripoti ikisema, wamewalisha panya chakula chenye mafuta mengi na kufanya utafiti. Wakagundua mafuta tumboni yamezalisha idadi kubwa ya protini maalumu ambayo inazifanya seli za kawaida kuwa dhaifu na kubadilika kuwa seli za saratani. Ikilinganishwa na mafuta ya chini ya ngozi, mafuta ndani ya maini yanaweza kuzalisha protini nyingi zaidi ya aina hiyo.

Baada ya hapo, watafiti wameweka mafuta yaliyokusanywa katika mwili wa binadamu kwenye mwili wa panya. Matokeo yameonesha kuwa mafuta yanazalisha protini nyingi zaidi ya aina hiyo, seli nyingi zaidi zinakuwa seli za saratani.

Utafiti umependekeza kuwa, watu wanatakiwa kuwa makini na mafuta yaliyomo ndani ya tumbo, kudhibiti kitambikwa kufanya mazoezi na kuzingatia ulaji vya vyakula visivyo na mafuta.

VIDEO: WAFANYAKAZI NAKUMATT WALALAMIKIA KUKOSA MSHAHARA

Chanzo: millardayo.com