Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jiko lateketeza majengo ya Hospitali

3041 Tew1 660x400 TZW

Mon, 12 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Moto ulizuka katika hospitali ya Mission ya Tenweek na kusababisha wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo kulazimika kukimbia wodi ili kuokoa maisha yao baada ya moto huo kuteketeza baadhi ya majengo

Hospitali  ya Tenweek ipo katika Jimbo Bomet nchini Kenya, ilishika moto baada ya jiko la hospitali hiyo kulipuka na kuteketeza maeneo ya karibu ikiwemo store ya chakula na mgahawa na baadhi ya vyumba ambayo viko karibu na kitengo cha waonjwa mahututi na wodi kuu.
Mkuu wa Polisi Jimbo la Bomet, Samson Rukunga amesema jeshi la polisi limejitahidi kudhibiti moto huo usiathri sehemu kubwa na kuwahi kuuzima na hakuna madhara yaliyotokea kwa binadamu.

Chanzo: millardayo.com