Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo la Mama na Mtoto lafikia asilimia 70 Mwanza

8ba0caa364f846e949cd42a3a073839a Jengo la Mama na Mtoto lafikia asilimia 70 Mwanza

Thu, 28 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MRADI wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure lenye urefu wa ghorofa tano ulioanza kujengwa oktoba mwaka 2017 hadi sasa umefikia asilimia 70 mpaka kukamilika.

Hayo yalielezwa wiki ikiyopita na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure, Dk Bahati Msaki wakati akisoma taarifa ya maendelo ya mradi huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima akiwa ziarani mkoani hapa.

Dk.Bahati alisema ujenzi huo unatarajiwa kugharimu Sh.bilioni 10.1 hadi kukamilika na inatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 261 kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Moses Urio alisema kutokana na eneo hilo kuwa na maji kulipelekea msingi kujengwa kwa muda mrefu na kuboreshwa kwa mahitaji, kubadilika kwa mchoro ambapo vitanda viliongezeka kutoka 100 hadi 261.

Aidha Dk Gwajima alimtaka mkaguzi wa majengo ya serikali kusimamia miradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu na kusisitiza ni vema wakandarasi wa miradi mbalimbali ya afya kufanya vikao na wajumbe ili kubadilishana mawazo wakati wa utekelezaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya nyamagana Dk Philis Nyimbi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema atahakikisha anafatilia kwa karibu ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na wananchi waweze kupata matibabu kwenye jengo hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz