Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Jengeni tabia kupima afya ya kinywa’

A787d38265f954795aaa18c4b6ce856a ‘Jengeni tabia kupima afya ya kinywa’

Thu, 28 Jul 2022 Chanzo: Habari Leo

Jamii imeshauriwa kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa mara kwa mara, kwani isipofanyika tiba ya uhakika kuna hatari ya kuwa chanzo cha magonjwa mengine.

Hayo yamesemwa leo Julai 28, 2022 jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa kliniki ya kinywa na meno iitwayo Afya Bora Complete Dentistry LTD, Dk Donna Ngirwa, wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo.

Anasema kliniki yake itajikita zaidi kueneza elimu kuhusu uhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya ya binadamu kwa ujumla.

Amesema kituo hicho kitatoa huduma zote za meno, ikiwemo usafishaji wa meno, kuweka meno ya bandia, mpangilio wa meno na huduma nyinginezo za tiba ya meno.

“Utafiti unaonyesha kuwa magonjwa mengi yakiwemo shambulio la moyo, kisukari, kiharusi, maambukizi katika mapafu na magonjwa mengine yana mahusiano wa karibu na maambukizi yaliyopo katika kinywa.

“Hivyo suala la afya ya kinywa ni muhimu sana lifanyike mara kwa mara,” amesema.

Chanzo: Habari Leo