Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Je, wajua kupenda sana ngono ni ugonjwa wa akili?

15155 Dk+CHRIS TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kwa wasomaji wangu kama kuna yeyote ambaye nimewahi kumuhudumia kwenye idara ya afya ya akili hususani kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na sonona (depression), basi bila shaka atakumbuka moja ya aina mbalimbali za ushauri kuhusiana tatizo hili.

Na ushauri huu sio mwingine bali ni kufanya vile vitu ambavyo unahisi kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha furaha yako. Yaani kupitia mambo hayo basi furaha yako huanzia hapo; ili mradi tu usivunje sharia.

Baadhi ya wagonjwa hawa, wamekuwa wakiniuliza maswali kama vile; “ kwa hiyo daktari ninaweza hata kushiriki tendo la ndoa kila ninapohisi kuwa dalili za sonona zinaninyemelea?” na jibu langu huwa ndiyo! Ili mradi tu tendo la ndoa lifanyike kwa usahihi na usalama.

Kisayansi, kushiriki tendo la ndoa na hasa na mtu ambaye amekuvutia kihisia, ni moja ya njia zinazosaidia kuuweka sawa mfumo wa afya ya akili na kumuondoa mtu kwenye hatari ya kupata au kuelemea na matatizo ya afya ya akili kama vile msongo wa mawazo na sonona.

Na ndio maana huwa tunashauri ni vyema ikafahamika kuwa, dhumuni la tendo la ndoa sio kuzaa tu, bali ni moja ya njia zinazotumika kustawisha vile vichocheo vya furaha ama kwa kitaalamu vinajulikana kama “feel-good hormones” na kumfanya mshiriki wa tendo la ndoa awe mwenye furaha.

Lakini kama ilivyo kwa jambo lolote, likifanyika kupita kiasi, hata kama ni jema linageuka na kuwa baya. Na ukweli huu upo pia hata kwenye suala hili la kushiriki tendo la ndoa na nikiwa kama daktari ninadhani ni wakati muafaka sasa jamii zikapata uelewa kuhusiana na jambo hili, hii ni kufuatia na taarifa zilizotolewa karibuni na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya kiafya (WHO),zikionya kuwa uhusiano mkubwa uliopo kati ya kupenda ngono kupita kiasi na magonjwa ya akili.

Mara nyingi ni vigumu sana kwa mtu mwenye matatizo ya akili kujigundua kama yeye ni mgonjwa wa tatizo fulani la afya ya akili na ndio maana hata kwenye kupenda ngono kupita kiasi ni vigumu kwa mtu kujitambua kuwa ni tatizo pasipokupatiwa ushauri .

Hivyo msomaji ni vyema leo ukatambua kuwa, kupenda sana kufanya ngono kupita kiasi ni tatizo la kiakili na ni vyema likachukuliwa kwa uzito kama yanavyotiliwa maanani matatizo mengine ya kiafya.

Tatizo kitaalamu linajulikana kama nymphomania kwa wanawake lakini pia kwa wanaume linajulikana kama satyriasis lakini kwa ujumla ni ile hali ya mtu kuwa na tamaa ya kushiriki tendo kupita kiasi.

Tatizo hili linakuja kwa sura mbalimbali pasipo mtu kujijua, lakini baadhi ya dalili kuu za tatizo hili ni pamoja na kupenda sana tabia ya kujichua, kuwa na washirika wengi au kuwa na idadi kubwa ya watu unaofanya nao ngono, kupenda sana kuangalia video za ngono, kupendelea kufanya ngono pasipo kutumia kinga, kupendelea kuwa karibu na sehemu ambayo kuna wafanya biashara ya ngono kutokana na ukweli kuwa utaweza kufanya ngono kirahisi na kwa maelewano madogo na pia kujikuta wakati mwingine unalazimika kusitisha kufanya shughuli muhimu na za kijamii ikitokea ili kufanya ngono.

Iwapo mtu atapitia dalili hizi basi dhahiri kuwa mtu huyu tayari ana tatizo la kiakili na anahitaji msaada wa awali ambao ni wa ushauri kutoka kwetu wahudumu wa afya, wanasaikolojia, lakini pia kutokwa kwa viongozi wa dini kabla hali hii haijamsababishia matatizo makubwa kama vile magonjwa ya maambukizi yatokanayo na ngono na matatizo mengine ya kifamilia na kijamii

Chanzo: mwananchi.co.tz