Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Je wajua binadamu hulala muda mfupi kuliko wanayama wengine?

Sleeping Binadamu.png Je wajua binadamu hulala muda mfupi kuliko wanayama wengine?

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda tunaotumia tukiwa macho na kulala ukilinganisha na jamaa zetu wakiwemo nyani huenda ulisaidia sana katika mabadiliko yetu. Katika usiku kavu, wawindaji wa San wa Namibia mara nyingi hulala chini ya nyota. Hawana taa za umeme au matoleo mapya ya filamu za Netflix ili kuwaweka macho.

Hata hivyo wanapoamka asubuhi, hawajalala saa nyingi zaidi ya mkaazi wa kawaida wa jiji la Amerika Kaskazini au Ulaya ambaye amekuwa macho akitazama simu zao. Kulingana na mwanaanthropolojia wa mageuzi David Samson wa Chuo Kikuu cha Toronto huko Mississauga, utafiti umeonyesha kuwa watu katika jamii zisizo za kiviwanda ambazo hukaribia sana na mazingira ambayo spishi zetu ziliibuka - hulala chini ya masaa saba kwa usiku.

Hii inashangaza unapozingatia jamaa zetu wa karibu kwamba mwanadamu hulala saa kidogo kuliko tumbili. Sokwe hulala takribani saa 9.5 kwa siku na nyani wenye vichwa vyeupe hulala kama masaa 13. Samson anaita hitilafu hii kuwa kitendawili cha usingizi wa mwanadamu.

"Inawezekanaje sisi ni nyani ambao hulala muda kidogo?" anauliza.

Usingizi unajulikana kuwa muhimu kwa kumbukumbu yetu, kinga ya mwili, na mambo mwngine ya afya yetu.

Mamilioni ya miaka iliyopita, babu zetu waliishi, na labda walilala, kwenye miti. Hata leo, sokwe na nyani wengine hulala kwenye vitanda au maeneo ya muda kwenye miti. Wanapinda au kuvunja matawi ili kuunda umbo la bakuli, ambalo wanaweza kutandika matawi ya majani (nyani kama sokwe pia wakati mwingine hujenga vitanda chini).

Wazee wetu walitoka kwenye miti ili kuishi chini na wakati fulani walianza kulala huko pia. Hii inamaanisha walilazimika kuacha faida zote za kulala kwenye miti, pamoja na usalama kutoka kwa wanyama wanaowinda kama vile simba.

Mabaki ya mababu zetu hayaonyeshi jinsi walivyokuwa wamepumzika. Ili kujua jinsi wanadamu wa kale walivyolala, wanaanthropolojia wametafuta ushahidi bora walio nao: jamii za kisasa zisizo za kiviwanda.

"Ni heshima kubwa na nafasi kubwa kufanya kazi na jumii hizi," anasema Samson, ambaye amefanya kazi na wawindaji wa Hadza nchini Tanzania, pamoja na vikundi mbalimbali nchini Madagascar, Guatemala na kwingineko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live