Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa akutwa na Ukimwi, Covid-19 na homa ya nyani

Chanjo Ya Ukimwi Vvu.jpeg Akutwa na Ukimwi, Covid-19 na homa ya nyani

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja Raia wa Italia anaaminika kuwa Mtu wa kwanza duniani kukutwa na virusi vya homa ya nyani, virusi vya corona pamoja na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi vyote kwa wakati mmoja.

Wataalamu wanasema ni nadra sana kupata Mgonjwa mwenye covid 19 pamoja na homa ya nyani kwa wakati mmoja na hakuna mfano unaojulikana wa Mtu kugunduliwa kuwa na maambukizo yote matatu kwa wakati mmoja.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 36 alirejea hivi karibuni Nchini Marekani akitokea Hispania ambapo ndani ya wiki moja baada ya kurudi alipata dalili ambazo ni pamoja na homa, koo, maumivu ya kichwa na pia kuanza kuona vipele visivyo vya kawaida kwenye mkono na mwili wake, imeripoti mitandao ya Marekani.

Haijajulikana hasa ni lini aliambukizwa kila kirusi lakini iliaminika kuwa ni ndani ya muda wa hivi karibuni huku rekodi zake zikionesha kuwa alikuwa ametibiwa kaswende mwaka 2019.

Mwanaume huyu ametibiwa homa ya nyani pamoja na covid 19 pamoja na kuanza rasmi kumeza dawa za VVU.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live