Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaffo, Gwajima wapewa siku 7

B90bae57f4db812af04ec628f97fb968 Jaffo, Gwajima wapewa siku 7

Thu, 28 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS John Magufuli ametoa siku saba kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima na Waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo wampe majibu ya kwa nini Mkoa wa Geita wanapunjwa madawa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo akizindua vituo vya afya vya Masumbwe na Mbogwe mkoani Geita ambapo alisema mwaka 2015 bajeti ya madawa mkoa wa Geita ilikuwa bilioni 2.35 mwaka 2020 ilikuwa bilioni 2.75.

Amsema anataka majibu ni kwa namna gani dawa zitaongezwa katika hospitali ya Masumbwe, Mbogwe na maeneo mengine.

"Inawezekana kuna upunjaji wa mgawo wa madawa katika Mkoa huu ikiwemo Masumbwe, bajeti ya madawa imeongezeka lakini madawa yanayotolewa hapa ni kidogo, Waziri wa Afya na wa TAMISEMI mnaopanga bajeti ya madawa mkakae ndani ya siku saba mlete jibu, "amesisitiza

Aidha Rais Magufuli amewashukuru wana Masumbwe na Mbogwe kwa kumpigia kura nyingi.

"Nawashukuru wana Masumbwe na wana Mbogwe kwa kura nyingi sana mlizonipa na kuniwezesha kuwa Rais, mlinipa mimi mkampa na Maganga awe Mbunge wa jimbo hili na mkawapa kura nyingi sana madiwani wa CCM asanteni sana"-

Chanzo: habarileo.co.tz