Dar es Salaam. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imepata msaada wa kifaa cha kupima moyo chenye uwezo wa kubaini asilimia 95 ya magonjwa ya moyo kwenye mwili wa binadamu.
Kitaa hicho kinachofahamika kitaalam kama Echo Machine kimetolewa na taasisi inayoshughulika na kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo ya Sach Canada.
Akizungumza leo Jumatano Mei 29, 2019 mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi amesema kifaa hicho kimekuja wakati muafaka kutokana na muda mrefu kushindwa kubaini matatizo ya moyo.
Amesema kinaweza kuhamishwa kutoka eneo moja kwenda jingine, kwamba kinaweza kupelekwa mikoani kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa huko.
Amebainisha kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kubaini mtoto mwenye matatizo ya moyo tangu akiwa tumboni mwa mama yake.
“Watoto wengi wanazaliwa wakiwa na matatizo ya moyo lakini kwa kifaa hiki mama mjamzito akichunguzwa kuanzia wiki ya 20, tatizo linaweza kubainika.”
Pia Soma
- Wanne kortini kwa kukutwa na nyama ya kiboko
- Kiongozi mbio za mwenge awapa somo watumishi wa umma
- Ilichokisema NEMC kuhusu mifuko ya plastiki
Mkurugenzi wa Sach Canada, Marni Brinder Byk amesema wanatambua juhudi za JKCI katika kukabiliana na matatizo ya moyo na ndio sababu wamewapatia kifaa hicho.