Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKCI yaokoa Sh bil. 51 matibabu ya moyo

2b14593f3811c693c0fb984d37ae7a27 JKCI yaokoa Sh bil. 51 matibabu ya moyo

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI), imeokoa kiasi cha Sh bilioni 51 baada ya wagonjwa wengi kutibiwa ndani ya nchi.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Prof. Mohammed Janabi, ameseishukuru serikali kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha huduma ya moyo nchini.

Prof. Janabi ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bodi ya taasisi hiyo, ambapo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alikuwa mgeni rasmi.

"Leo aina 30 za upasuaji zinafanyika, tunapeleka wataalamu kusoma nje tunamshukuru serikali,” amesema.

Amesema idadi ya wagonjwa inaongezeka, amabapo tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo jumla ya wagonjwa 605,933 wanehudumiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live