Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKCI watoa ofa ya kupima moyo baada ya ushindi wa Stars

48519 Pic+moyo

Mon, 25 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imetoa ofa kwa wagonjwa wa nje kupima kwa nusu ya bei katika masaa nane ili kushangilia ushindi wa Taifa Stars.

Vipimo vilivyo kwenye ofa hiyo ni ECHO, kipimo kinachochunguza namna moyo unavyofanya kazi na ECG, kipimo kinachotazama umeme wa moyo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Machi 25, 2019 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano JKCI, Anna Nkinda amesema taasisi hiyo ina kila sababu za kuungana na Watanzania kushangilia ushindi wa timu yao.

Amesema kwa kawaida vipimo vinavyotolewa hugharimu zaidi ya Sh120,000 kwa wagonjwa binafsi huku rufaa ikiwa 65,000 pamoja na kumuona daktari.

"Mpaka sasa tumepata watu zaidi ya 450 wanaoendelea kufanyiwa vipimo hivi kwa nusu bei na baada ya vipimo wataingia kwenye mfumo wa kawaida wa matibabu," alisisitiza.

Nkinda ameongeza idadi ya wagonjwa wa moyo katika taasisi hiyo imekuwa ikiongezeka kila mwezi kutokana elimu inayoendelea kutolewa kwa jamii.

"Kwa siku tulikua tunapokea wagonjwa 100 hivi sasa wamefika 250 mpaka 300 hii inaonyesha watu wana uelewa," amesisitiza .

Mmoja wa watu waliojitokeza kupima Idrisa Ally alisema ofa ya nusu bei kwa vipimo vya moyo imemfanya apime afya yake.

"Nimekuja kwa sababu huwa nina dalili za uchovu mara kwa mara, kwa hiyo nimekuja kujua shida yangu," alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz