TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imefanikiwa kumfanyia upasuaji wa moyo na kubadilisha mshipa mkubwa wa damu na kuweka chuma mbadala, bila kumuongezea damu wala kusimamisha moyo wa mgonjwa Ayubu Ngonyani (24) ambaye ni muumini wa Jumba la Ufalme wa Mashahidi wa Yehova.
Mgonjwa huyo alikataa kufanyiwa upasuaji huo kwa kuongezewa damu kutokana na imani yake licha ya kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo ambalo lilihitaji upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo bila kumuongezea damu.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi amesema uchunguzi ulibaini mshipa mmoja wa damu kwenye moyo (valve) ulikuwa imeharibika mno.