Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKCI Kushirikiana na Madaktari toka Czech

Cki Jengo la JKCI

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ipo mbioni kuanzisha ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech.

Akizungumza baada ya kufanya ziara JKCI jana Jijini Dar es Salaam Mkuu wa msafara wa madaktari sita kutoka nchini Czech Miroslav Homza amesema kuwa lengo kuu wa madaktari hao kufika JKCI ni pamoja na kuangalia jinsi ambavyo wataweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo ikiwa ni njia ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Czech.

“Tumefika hapa JKCI na kukutana na uongozi kujadilina juu ya uwezekano wa madaktari kutoka JKCI na wale wa Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri wa watu wa Czech kuweza kubadilishana uzoefu katika kutoa huduma za matibabu ya moyo haswa upande wa upasuaji wa moyo”,

“Sambamba na kutoa huduma za matibabu ya moyo pia tutaangalia namna gani tunaweza kushirikiana upande wa utafiti katika masuala ya magonjwa ya moyo kati yetu na Tanzania”, alisema Homza.

Aidha Homza amesema kuwa katika ushirikiano huo Czech itaangalia kama kuna uwezekano wa wagonjwa ambao wapo Tanzania na wanahitaji huduma za matibabu ya kina kuchukuliwa na kupelekwa Jamhuri ya watu wa Czech kwa ajili ya matibabu hayo kwani Czech inatoa huduma za matibabu ya hali ya juu na kwa gharama nafuu tofauti na nchi nyingine duniani.

Akizungumzia ushirikianao wa kutoa huduma za matibabu ya moyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema kuwa JKCI imekua ikishirikiana na madaktari kutoka nchi mbalibmali ikiwa ni sehemu ya kuongeza uzoefu na kutoa hudama bora na za kibingwa za matibabu ya moyo.

“Leo tumepokea madaktari kutoka Jamhuri ya watu wa Czech ambao wamefika kujadiliana nasi namna ambavyo tutashirikiana katika kubadilishana uzoefu wa kutoa huduma za matibabu ya moyo, Tumekubaliana kuandaa makataba wa makubaliano ambao utatuongoza katika kushirikiana na kufaidia katika kubadilishana uzoefu huo”, alisema Prof. Janabi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live