Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya Muuguzi kufumua jeraha mgonjwa kisa malipo, Waziri Gwajima atoa namba

Trtrrrrrr 660x400 Ishu ya Muuguzi kufumua jeraha mgonjwa kisa malipo, Waziri Gwajima atoa namba

Sat, 4 Sep 2021 Chanzo: millardayo.com

Wizara ya Afya imesema imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii inayozunguka mitandaoni kuwa, Mtaalamu wa Afya katika kituo ambacho bado hakijatambuliwa amemshona Mgonjwa jeraha kisha akalifumua kutokana na Mgonjwa huyo kushindwa kulipia gharama za matibabu.

Wizara ya Afya imesema imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii inayozunguka mitandaoni kuwa, Mtaalamu wa Afya katika kituo ambacho bado hakijatambuliwa amemshona Mgonjwa jeraha kisha akalifumua kutokana na Mgonjwa huyo kushindwa kulipia gharama za matibabu. Wizara ya Afya imesema ikiwa hili limetokea nchini Tanzania, basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu, hivyo Wizara inaomba wenye taarifa za wapi huku au kituo gani wawasilishe mara moja kwa namba ya huduma kwa mteja 199 ya Wizara ya Afya au watume ujumbe mfupi kwenye namba ya Waziri wa Afya ya 0734124191.

Chanzo: millardayo.com