Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Incubator ya watoto njiti ina changamoto kuliko faida - Waziri Gwajima

A260b09f56f566ccc3ca49e19ca0642d Incubator ya watoto njiti ina changamoto kuliko faida - Waziri Gwajima

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIFAA cha kusaidia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya wakati au wenye uzito pungufu kuwapatia joto (incubator), kimebainika kuwa na changamoto nyingi kuliko faida, hatua ambayo serikali imeshauri hospitali zianzishe vyumba maalumu kwa ajili ya matibabu ya watoto wachanga.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Norah Mzeru (CCM), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima alisema ili kupunguza vifo vya watoto wachanga, wizara kwa kushirikiana na wadau, inasisitiza kila hospitali kuanzisha vyumba maalumu kwa ajili ya matibabu ya watoto wachanga kuendana na mwongozo wa kitaifa.

Katika swali lake, Mbunge Mzeru alitaka kufahamu mpango wa serikali wa kuweka mashine za incubator za kutosha nchini ili kuzuia vifo vya watoto.

“Hadi sasa tuna takribani incubator 214 nchi nzima kwenye ngazi ya hospitali mbalimbali. Hata hivyo tafiti zimeonesha kuna changamoto nyingi za kutumia “incubator” kuliko faida,” alisema.

Alifafanua kwamba vifaa hivyo vimebabisha kusambaa kwa magonjwa kutoka mtoto mmoja aliyelazwa humo awali kwenda kwa mwingine atakayefuatia kulazwa .

Alisema pia hakuna ukaribu wa mama aliyejifungua na mtoto aliyewekwa kwenye kifaa hicho.

Alisema matumizi ya kifaa hicho katika mazingira ambayo umeme si wa uhakika muda wote pia ni changamoto pia.

Chanzo: www.habarileo.co.tz