MIKOA mitano imepiga hatua katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria nchi ambapo imetajwa kuwa na kiwango chini ya asilimia moja.
Mikoa iliyotajwa ni Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Iringa na Manyara.
Akizungumza katika kikao kazi cha kwanza cha Wabobezi wa kudhibiti wadudu wanaoeneza magonjwa, Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Leonard Subi alisema kuwa mikoa mingine ina kiwango cha kati cha maambukizi hayo ya malaria.
Aidha, Dk Subi alisema pia wapo nzi weusi ambao wanaeneza ugonjwa wa usubi hususani kwenye mikoa ya Mbeya (Tukuyu), Morogoro (Mahenge) na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Iringa.