Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi ya wanaume wanaofunga uzazi kuongeza – madaktari

Idadi Ya Wanaume Wanaofunga Uzazi Kuong Idadi ya wanaume wanaofunga uzazi kuongeza – madaktari

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Idadi ya wanawaume wanaotumia njia ya kufunga uzazi ya kudumu (vasectomy) inatarajiwa kuongezeka zaidi, kuliko inavyoripotiwa kwa sasa, wanasema madaktari wa Uingereza waliofanya utafiti kuhusu suala hilo.

Madaktari hao wanasema baada ya kufanyiwa upasuaji wa kufunga uzazi, wanaume wanaweza kuhisi maumivu kidogo , lakini wanasema ni nadra kwa wanaume waliofunga uzazi kwa njia hiyo kupata madhara makubwa ya kiafya.

Upasuaji wa kufunga uzazi kwa njia ya vasectomy, huchukua dakika 15 pekeeImage caption: Upasuaji wa kufunga uzazi kwa njia ya vasectomy, huchukua dakika 15 pekee.

Kundi la madaktari hao lilitoa matokeo ya utafiti wake katika kongamano la matibabu lililomalizika Alhamisi Milan nchini Italia, baada yakuwafanyia utafiti wanaume 94,000 ambao walifungwa uzazi kwa njia ya vasectomy.

Upasuaji wa kufunga uzazi kwa njia ya vasectomy, ambapo mwanaume hudungwa sindano ya ganzi, huchukua dakika 15 pekee.

Kwa ujumla takwimu zinaonyesha kuwa wanaume wengi bado hawajitolei kufanyiwa upasuaji wa vasektomi kama njia ya kufanya uzazi wa mpango, zaidi kutokana na imani zinazozingira njia hii.

Ufungaji wa kizazi kwa wanaume ni nini?

Njia ya kufunga uzazi kwa wanaume ni njia ya uzazi wa mpango ambayo hufanywa kwa njia ya upasuaji kukata au kufunga mirija inayosafirisha mbegu za uzazi za mwanaume, ili kuzuia mwanamke asipate mimba.

Upasuaji mara nyingi hufanywa kwa muda wa dakika takriban 15, mgonjwa huwa macho lakini huwa hapati maumivu yeyote.

Njia hii inafanya kazi ya kuzuia mimba kwa silimia 95. Njia ya kufunga uzazi kwa wanaume haiathiri nguvu za kiume au uwezo katika tendo au kulifurahia tendo.

Mwanaume ataweza hayo yote,isipokuwa hataweza kumpa mwanamke ujauzito. Njia hii haizuii mwanaume dhidi ya maradhi ya zinaa, kama mipira ya kiume ambayo inaelezwa kuwa njia ya kuaminika kwa asilimia 98 ikiwa itatumika vyema.

Chanzo: Bbc