Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi maambukizi Covid-19 yapungua

CORONA CHANJO?fit=660%2C371&ssl=1 Idadi maambukizi Covid-19 yapungua

Wed, 30 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifello Sichalwe, amesema idadi ya maambukizi ya virusi vya corona vimepungua nchini.

Amesema awali kwa siku wastani wa watu 138 walikutwa na maambukizi corona, lakini sasa ni watu watano tu.

Amesema takwimu za matokeo ya upimaji katika impungua kutoka watu 138 kwa siku mwezi Desemba 2021 hadi watu watano kwa siku Machi 20, 2022.

Pia amesema wizara inaendelea kufatilia tabia za anuwai za virusi vinavyosababisha Covid-19 na kubaini kuwa hakuna kirusi mpya nchini zaidi ya Omicron.

Dk Sichalwe ameeleza kuwa wizara inashauri kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya Covid-19 katika vituo vya kutolewa huduma za afya na inawakumbusha kukamilisha dozi ili kupata kinga kamili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live