Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huu ndiyo umuhimu wa kula karoti

65765 Karoti+pic

Sat, 6 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Virutubisho vingi tunavipata katika matunda, mboga za majani, samaki, nyama na vyakula vingine vingi huku tukitumia karoti kama kiungo katika mapishi.

Licha ya karoti kuzuia maradhi yanayosababishwa na kasoro ya ugawanyikaji wa seli mwilini, watu hawajui thamani yake katika ulaji unaofaa.

Mtaalamu wa Lishe kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Scholastica Mlinda anasema ulaji wa karoti husaidia kuondoa sumu mwilini na kuongeza kinga ya mwili.

Mlinda anasema karoti ina vitamin ambayo husaidia kusafirisha mafuta mwilini na kuboresha afya ya ngozi ya mtumiaji.

Pia, ina vitamin A ambayo huboresha uwezo wa kuona na hulinda macho kukumbwa na matatizo yanayotokana na uzee.

Karoti ni chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zenye virutubisho ambazo husaidia kumeng’enya chakula na kurahisisha upatikanaji wa haja kubwa.

Pia Soma

Anasema pia hulikinga tumbo na magonjwa hasa kuzuia saratani ya utumbo na huimarisha afya ya kinywa.

Mlinda anasema ulaji wa karoti hufanya kinywa kuwa chenye harufu nzuri na huimarisha fizi zisishambuliwe na magonjwa ya kinywa.

“Karoti unaweza kuitengeneza juisi, saladi kwa kuchanganya na matunda, mbogamboga au kachumbari, lakini unaweza kuitumia kama kiungo katika mapishi yako.” Mbali na faida hizo, anasema kiungo hicho kinapokuwa mwilini husaidia kusaga sumu zilizopo katika ini na kusafisha kibofu.

Anasema pia husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa kuwa carotenoids iliyopo ndani ya karoti husaidia kudhibiti kiwango cha sukari.

Ni muhimu kula karoti katika kila mlo ili kupata kuupa mwili nguvu na kuepuka kupata magonjwa ya kinywa na saratani ya utumbo mpana.

Makala haya yameandikwa na mwandishi wa gazeti hili Hadija Jumanne

Chanzo: mwananchi.co.tz