Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huu ndio ukubwa wa Hospitali inayojengwa Geita

MAJENGOAA Huu ndio ukubwa wa Hospitali inayojengwa Geita

Mon, 11 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kupokea wagonjwa 800 kwa siku na kulaza wagonjwa 500 kwa wakati mmoja. Akiongea kwenye eneo la ujenzi mkoani Geita, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani humo Dkt Bryan Mawala amesema awamu ya kwanza inajumuisha ujenzi wa majengo manne.

Jengo la kwanza ni OPD au maarufu kama wagonjwa wa nje lenye ukubwa wa mita za mraba 3500 na Jengo la pili ni ghorofa lenye mita za mraba 7668, ambapo juu litakuwa na vyumba vya upasuaji.

Kwa mujibu wa maelezo ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ujenzi huo unatakiwa kukamilika Oktoba 30, 2020 na utagharimu Bilioni 2.56.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live