Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma ya mionzi hospitali ya Haydom kuinufaisha mikoa sita

74080 Mionzi+pic

Tue, 3 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Haydom. Wagonjwa wa saratani waliopo katika Mikoa sita ya Tanzania wataanza kupata huduma ya mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Haydom mkoani Manyara.

Mikoa hiyo ni Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Arusha na Simiyu kutokana na hospitali ya Hydom kununua mashine mpya ya mionzi baada ya iliyokuwa awali kuharibika.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 3, 2019 mkurugenzi wa tiba wa hospitali hiyo, Dk Emmanuel Nuwass amesema Sh800 milioni zimetumika kununua mashine hiyo.

Amebainisha kuwa watu wengi wana uhitaji mkubwa wa huduma hiyo, kwamba wapo baadhi katika mikoa hiyo wanalazimika kusafiri umbali wa kilomita 400 hadi 500 kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza au KCMC mkoani Kilimanjaro.

Amebainisha kuwa takribani miaka miwili hospitali hiyo haikuwa na mashine hiyo na kuwapa wakati mgumu waliokuwa wakihitaji huduma hiyo.

 "Tunawashukuru wadau wote waliwezesha hadi mashine hii kufika Haydom na tunatarajia hivi karibuni Waziri wa Afya,  Ummy Mwalimu atakuja kutuzindulia rasmi," amesema Dk Nuwass.

Pia Soma

Advertisement   ?
Mtaalamu wa mionzi wa hospitali hiyo, Paul Fissoo amesema mashine hiyo mpya ina uwezo mkubwa ikilinganishwa na iliyoharibika.

Mkazi wa Haydom, Catherine Faustine amesema takribani miaka miwili wagonjwa wengi hasa wasio na kipato wameshindwa kuchunguzwa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kwenda hospitali za mbali zinazotoa huduma hiyo.

Hospitali ya Haydom inahudumia wagonjwa 105,296 wa nje na 14,020 wa ndani kwa mwaka.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz