Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma ya kiti mwendo yaanzishwa kituo cha daladala Muhimbili

KITIMWENDO Huduma ya kiti mwendo yaanzishwa kituo cha daladala Muhimbili

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanzisha huduma ya kubeba wagonjwa wasioweza kutembea kutoka kwenye kituo cha daladala kilichopo nje ya geti la kuingilia hadi katika maeneo ya kutolea huduma kwa kutumia viti mwendo (Wheel chairs)

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa MNH, Bi. Redempta Matindi amesema kuwa huduma hiyo ni muhimu kwa kuwa wapo wagonjwa wasiojiweza kabisa kutembea wenyewe.

"Sisi kama watoa huduma tumeona ni vema kuanzisha huduma hii kuwasaidia mwendo wagonjwa ili wafike kwenye maeneo ya kutolea huduma wakishafika huko wanakutana na watoa huduma wa maeneo husika" amesema Bi. Redempta

Amesema huduma hizo zinatolewa na waliokuwa waraibu wa dawa za kulenya ambao wanaendelea na tiba ya Methadone ili kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live