Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma mpya ya tiba ya ubongo kupitia mshipa wa paja yaja Tanzania

68740 Pic+tiba

Mon, 29 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) nchini Tanzania, inatarajiwa kuanza kutoa matibabu ya upasuaji wa ubongo kupitia mshipa wa damu wa paja badala ya kufungua fuvu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai 29, 2019 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile wakati akifungua kongamano la kimataifa la mafunzo ya upasuaji wa ubongo kwa mbinu za kisasa.

Amesema tayari wataalamu wameshapatiwa mafunzo ya miezi mitatu nchini China.

"Sh16.5 bilioni zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya miezi miwili iliyopita tumetoa Sh7.9 bilioni kwa ajili ya kununua vifaa vya kisasa na hivyo Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kutoa matibabu ya upasuaji wa kufika kwenye ubongo kupitia mshipa wa paja ni mafanikio makubwa na serikali tumeendelea kufanya kuhakikisha tunaondoa kabisa wagonjwa wanaokwenda nje," amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respicious Boniface amesema mchakato uliopo sasa ni kununua vifaa na utakapokamilika wanatarajia kuanza huduma hiyo mpya ifikapo Oktoba mwaka 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz