Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma bobezi zaidi ya 35 Muhimbili zapunguza rufaa

Huduma Bobezi Zaidi Ya 35 Muhimbili Zapunguza Rufaa.png Huduma bobezi zaidi ya 35 Muhimbili zapunguza rufaa

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upatikanaji wa huduma za ubingwa bobezi zaidi ya 35 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila na Upanga) zimepunguza rufaa za matibabu nje ya nchi ikiwa ni jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Huduma hizo ni upandikizaji wa figo kwa njia ya matundu, upandikizaji wa uloto, uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, upandikizaji wa nyonga na magoti, kuvunja mawe kwenye figo kwa kutumia mawimbi mtetemo pamoja na kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa kupitia matundu ya pua.

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema hayo alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mkoani Dar es Salaam leo akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ismail Rumatila na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dkt. Hamad Nyembea.

"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi yake kubwa kwa kutujengea majengo, kununua vifaa na vifaa tiba katika miaka hii mitatu. Sekta ya afya imekua sana nchini hasa katika huduma hizi za ubobezi. Sasa jukumu ni la kwetu sisi watumishi kuwahudumia watanzania kwa kuwapa huduma bora." Amesema Waziri Mhagama

Chanzo: www.tanzaniaweb.live