Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali za rufaa sasa kuwa chini ya Wizara ya Afya

10575 Ummy+pic

Tue, 3 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, wazee na Watoto, Ummy Mwalimu imesema hospitali zote za rufaa za mikoa zitakuwa chini ya wizara hiyo.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kapasi ya Mloganzila (Mamc).

Akizungumza leo Jumatatu Julai 2, 2018 katika ziara aliyofanya katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Ummy  amesema wizara hiyo imepokea  jumla ya hospitali 28 kutoka Ofisi ya Rais, Tamisemi zenye jumla ya vitanda 7,474 na watumishi 8,671.

Amezitaja hospitali hizo kuwa ni Maunt Meru (Arusha), Dodoma General (Dodoma), Kitete (Tabora), Shinyanga, Geita, Singida na Mpanda (Katavi), Mawenzi (Kilimanjaro), Bombo (Tanga), Morogoro na Ligula(Mtwara).

Nyingine ni Sokoine (Lindi), Maweni (Kigoma), Sekou Toure (Mwanza), Mwananyamala, Amana na Temeke (Dar es Salaam), Songwe na Kibena (Njombe), Iringa na Tumbi(Pwani), Sumbawanga(Rukwa), Bariadi (Simiyu), Musoma (Mara), Songea (Ruvuma), Mbeya na Babati (Manyara) na Bukoba (Kagera).

Amesema hospitali hizo zitawajibika moja kwa moja kwa wizara kupitia kwa katibu mkuu kwa masuala yote ya utawala na kitaalam.

Huku akieleza upungufu unaozikabili hospitali hizo, ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti amesema, “wizara  imeandaa mpango wa kuboresha huduma katika hospitali za rufaa za mikoa wenye muelekeo wa kuzipatia  mamlaka ya kujisimamia na kujiendesha.”

“Lakini  zikiwa chini ya uangalizi wa karibu wa Wizara ili kuongeza kasi ya uwajibikaj na kuleta matokeo ya haraka katika kufikisha huduma bora.”

Chanzo: mwananchi.co.tz