Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali yakanusha kununua figo

Figooo Data 1 Hospitali yakanusha kununua figo

Tue, 21 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali kuu ya umma nchini Kenya inasema kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu wanaouliza na kujitolea kuuza figo zao.

Katika chapisho la Facebook, Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ilisema " Figo yangu ni pesa ngapi?" lilikuwa swali lililoulizwa zaidi kupitia ujumbe kwenye ukurasa wao.

Hospitali hiyo hata hivyo ilishauri kwamba viungo vya mwili vinaweza kutolewa kwa wagonjwa.

"Tafadhali kumbuka kuwa uuzaji wa viungo ni marufuku kabisa na ni kinyume cha sheria. Unaweza tu kuchangia kwa hiari yako," ilisema.

Bango la hospitali hiyo linaangazia hatua za kukata tamaa ambazo watu wanafikiria huku kukiwa na ongezeko la bei ya chakula na mafuta.

Benki ya Dunia mapema mwezi huu ilionya kuwa Afrika mashariki ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na mdororo mkubwa wa uchumi kwa sababu ya vita vya Urusi nchini Ukraine na janga la Corona

Chanzo: www.tanzaniaweb.live