Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya wilaya ya Kisarawe yatajwa kuwa na uhaba wa damu

Kutoa Damu Onyo Hospitali ya wilaya ya Kisarawe yatajwa kuwa na uhaba wa damu

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu salama katika Benki yake ya damu ambapo zaidi ya chupa 35 zinahitajika kwa wiki kwa ajili ya kuwahudumia akina mama wajawazito na manusura wa ajali mbalimbali wanaofika hospitalini hapo

Akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu, Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Martha Chawe amesema hospitali ina uhitaji mkubwa wa damu kufuatia kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wanaofika kwaajili ya kufanyiwa upasuaji ambapo kwa siku hulazimika kutumia zaidi ya chupa tano kwa wagonjwa wenye uhitaji.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa damu katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe baadhii vijana kutoka chama cha mapinduzi UVCCM wilaya wamejitokeza kuchangia damu kama sehemu ya kutambua mchango wao katika kuokoa maisha ya wagonjwa.

Akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Kisarawe katika zoezi la uchangiaji damu afisa tarafa ya Sungwi KASMIR KOMBO Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Kisarawe akawataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ifikapo Agosti 23, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live