Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Saint. Joseph kuanza kusafisha figo

4e50b7310e6ae2a568239ca923813f35 Hospitali ya Saint. Joseph kuanza kusafisha figo

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

HOSPITALI teule ya St Joseph katika halmashauri ya manispaa ya Moshi, imeanzisha rasmi kitengo cha kusafisha figo ili kukabiliana na wimbi la kuongezeka kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ndani na nje ya manispaa hiyo.

Hospitali hiyo ilianza kupokea jumla ya wagonjwa saba wenye matatizo ya Figo mwaka 2017 na kuongezeka hadi kufikia wagonjwa 104 mwaka huu, jambo ambalo limeilazimu hospitali hiyo kuanzisha kitengo hicho rasmi.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Hellen Kyilyosodu, alisema hayo akitoa taarifa fupi ya huduma zinazotolewa katika hospitalini hiyo inahudumia zaidi ya watu 222,225 ikiwa kama hospitali ya rufaa katika ngazi ya wilaya.

Dk Kyilyosodu alisema kitengo cha figo katika hospitali hiyo kimejengwa kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la African Health Network, uongozi wa hospitali hiyo pamoja na shirika la masista wa bibi yetu wa Kilimanjaro.

Alisema kitengo hicho kimegharimu zaidi ya Sh Mil 882.3 ambapo wahisani walitoa kiasi cha Sh Mil 803, Shirika la masista wa bibi yetu wa Kilimanjaro Sh Mil 57.7 huku hospitali ya St Joseph ikitoa Sh Mil 21.

Mganga huyo alisema hospitali hiyo yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 162 huku ikitibu wangonjwa wa nje wastani wa wagonjwa 100 hadi 150, imeanzisha kitengo cha figo ili kupunguza msongamano katika hospitali ya rufaa ya kanda ya KCMC

Alisema kwa sasa hospitali ipo tayari kupokea wagonjwa kwani tayari ina vifaa tiba vyote vinavyohitajika ambapo sasa ina vitanda vinne kwa ajili ya wagonjwa wa kawaida na vitanda vitatu kwa ajili ya wagonjwa wenye magonjwa ya kuambukiza.

Chanzo: www.habarileo.co.tz