Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Rufaa Shinyanga yapigwa jeki vifaa corona

MNEC.webp Hospitali ya Rufaa Shinyanga yapigwa jeki vifaa corona

Thu, 4 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa mkoani Shinyanga (MNEC), Gasper Kileo, ametoa vifaa vya kisasa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Vifaa vilivyotolewa leo na mjumbe huyo ni kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki, masinki matano, tenki la maji lenye ujazo wa lita 1,000, vitakasa mikono, barakoa, gloves, pamba ,cord clamp na pulse Oximeter, vyenye thamani ya Shilingi Milioni 8.

Alisema ametoa vifaa hivyo ilikuiongezea nguvu Serikali ya mkoani Shinyanga, dhidi ya kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

“Ninaishukuru Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais wetu John Magufuli namna ilivyopambana na ugonjwa wa huu wa Corona (COVID – 19), na sisi tutaendelea kumuunga mkono na ndio maana nimetoa vifaa hivi ili kuendeleza mapambano,” alisema Kileo.

“Nawapongeza pia Madaktari wetu wote nchi nzima wamepambana kuhudumia wagonjwa wa corona, na Mungu ametusaidia tumeweza, naomba tuendelee kupambana mpaka pale Amiri Jeshi Mkuu Dk. John Pombe Magufuli atakaposema silaha zetu tuziweke chini”, ameongeza.

Aidha akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, amemshukuru mjumbe huyo wa Nec kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali, katika mapambano ya kukabiliana na janga hilo la virusi vya corona.

Pia aliwataka wananchi mkoani humo kuendelea kutekeleza maagizo ya Serikali kwa kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na majitirika, ili kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo vya corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live