Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Rufaa Mbeya yapewa cheti kutibu watoto miguu kifundo

Zas.webp Hospitali ya Rufaa Mbeya yapewa cheti kutibu watoto miguu kifundo

Thu, 4 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi inayo toa huduma kwa watoto wenye ulemavu wa mguu kifundo (TCCO) kwa kushirikiana na Shirika la msaada kwa watoto wenye nyayo zilizopinda (Clubfoot)- MIRACLE FEET leo wamekabidhi cheti cha shukrani kwa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya-

kwa kuendelea na utoaji wa huduma za matibabu ya watoto wenye tatizo la miguu kifundo kwa Nyanda za Juu Kusini.

Akikabidhi cheti hicho Mratibu Msaidizi wa TCCO Nyanda za Juu kusini, Ainael Sarinjo, ameipongeza hospitali kwa hatua ilizozichukua katika kukabiliana na janga la virusi vya corona huku wakiendelea kutoa huduma kwa watoto wenye miguu kifundo.

Amesema kuwa Taasisi yao wameridhishwa na kufurahishwa na hospitali kutositisha huduma za matibabu kwa watoto wenye miguu kifundo kwasababu tu ya corona.

Aikipokea Cheti hicho kwa niaba ya viongozi na watumishi wa hospitali ya MZRH, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali Dkt. Godlove Mbwanji ameishuukuru Taasisi ya TCCO kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na watumishi wa hospitali hasa katika idara ya Phisiotherapi kwa kuona kwamba matibabu kwa watoto ni lazima yaendelee hata katika kipindi hiki cha COVID-19.

“Tunaishukuru sana TCCO kwa kutambua mchango wa hospitali yetu kuliona hili, nasi tunarudisha pongezi hizi kwa Mh. Raisi John Pombe Makufuli kwa sababu katika ngazi ya Taifa katutia moyo sana, na kufanya mambo yaendelee hata katikati ya hili janga ambalo limekua likiisumbua dunia nzima, na hii imefanya huduma za wagonjwa wengine ikiwa ni pamoja na watoto wenye mguu kifundo kuendelea kupata huduma kama inavyotakiwa” – Dk. Mbwanji.

Hospitalii ya Rufaa ya Kanda Mbeya inatoa huduma ya kliniki na matibabu ya miguu kifundo au nyayo zilizopinda ambao ni ulemavu unaotokana na matatizo ya mifupa na misuri ambayo ni wakuzaliwa nao na unaweza mpata mototo yeyote duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live