Sat, 14 Nov 2020
Chanzo: habarileo.co.tz
WAFANYAKAZI wapya 68 wameajiriwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika ngazi mbalimbali.
Mkuu wa Idara ya Ajira na Mafunzo wa Muhimbili, Abdallah Kiwanga alisema hospitali imeajiri wataalamu wa macho, tiba ya viungo, wahudumu wa afya, wauguzi, wauguzi wasaidizi, watunza kumbukumbu na wataalamu wa maabara.
Uongozi wa hospitali umewapatia mafunzo ya maadili ya utumishi wa umma na kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Katika mafunzo hayo, wafanyakazi hao wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi na kutojihusisha na rushwa kwani inachelewesha na kuzuia utoaji bora wa huduma za afya.
Chanzo: habarileo.co.tz