Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Moyo "JKCI" na mbinu mpya ya chanjo ya COVID-19

20359b3d2edd3a134b6fee252bff78ff Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohhamed Janabi

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

IKIWA ni Siku ya tatu leo tangu kuanza kutolewa kwa chanjo ya ugonjwa wa Uviko -19 nchi, Mamia ya watu wameendelea kujitokeza kupata chanjo hiyo katika jiji la Dar es Salaam.

Katika kituo kilichopo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) licha ya kutoa chanjo elimu ilitolewa kabla ili kuelewa na kufanya maamuzi sahihi.

Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohhamed Janabi alisema mwitikio wa watu ni mkubwa huku kwa siku ya juzi takribani watu 250 walijitokeza kupata chanjo.

"Tulipewa jukumu la kutoa chanjo kwa viongozi wastaafu ,waliokuwa kazini na kwa wananchi wa kawaida ambao wamekisajili mtandaoni na tukiangalia mwitikio ni mkubwa jana walikuwa watu 250 lakini leo namba ni kubwa zaidi.

"Utaratibu ni kwamba wakifika tunatoa elimu kuhusu Covid ni kitu gani?chanjo imepatikanaje?, hali ilivyo kwa sasa Duniani? wangapi wanapata chanjo?, bara la Afrika limepata chanjo kiasi gani? madhara ya chanjo?faida za chanjo baada ya kufanya hayo yote tunaruhusu maswali.

Alisema baada ya mtu kuelewa anajaza fomu kwa hiari kuwa ameelewa maelezo yetu yote tuliyoyatoa na kama imeeleweka baada ya hapo anasaini kupata chanjo kwa hiari yake.

"Kwa siku ya jana mpaka leo kuna watu watatu pekee ndo hawakuchanjwa kwasababu moja alikutwa na homa lakini wote waliobakia wamechanjwa

Baada ya chanjo taratibu za kiafya ni lazima ifuatwe kama kuvaa barakoa,kunawa mikono kwa maji tiririka lazima zifuatwe .

"Kwasababu hamna chanjo Duniani ambayo ni asilimia 100 kwamba tofauti ni kwamba asiyechanjwa ugonjwa unaweza kuwa na athari zaidi ukilinganisha na aliyechanja,"alifafanua.

Alibainisha kuwa Chanjo ni kitu bora imesaidia wengi ambapo kuna chanjo 9 ambazo zinakinga magonwa 13 na kufanya wagonjwa wamekuwa wachache au hawapo kabisa.

"Chanjo ya Johnson uhifadhi wake ni rahisi kwenye friji ya kawaida na inafaa kwa mazingira yetu kwenye friji inakaa miezi minne na nusu muhimu tuendelee kumuomba Mungu kila mtu kwa imani yake na tuchukue tahadhari za kiafya,"alishauri.

Wakizungumza na HabariLEO wananchi waliopata chanjo walisema wanafurahia hatua ya serikali matumizi yake kwani imewafanya kujihisi kuwa salama zaidi.

Aisha Shariff Mkazi wa Mbezi beach aliyepata chanjo JKCI alisema mara baada ya kupata chanjo hajaona mabadiliko katika mwili wake.

Mwananchi mwingine Abdulatif Omary (50) Mkazi wa Magomeni Mapipa aliyepata chanjo kituo cha afya cha Magomeni alisema ameamua kuchanja kwasababu ugonjwa upo hivyo kuchanja ni muhimu.

"Nawashauri watu waje kwani watakapopata ugonjwa mkali itawagharimu zaidi hivyo wawahi kupata chanjo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz