Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Mount Meru yapata vifaa vya mifupa

Hospitaliipiic Data Hospitali ya Mount Meru yapata vifaa vya mifupa

Thu, 2 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru imepata vifaa tiba vya upasuaji wa mifupa kwa mara ya kwanza vyenye gharama Sh400 milioni.

Akikabidhiwa vifaa hivyo, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Alex Ernest amesema kabla ya ujio wa vifaa hivyo wagonjwa waliopata ajaliĀ  walikuwa wanapewa huduma ya kwanza na kuhamishiwa hospitali nyingine.

Vifaa hivyo vimetolewa na Serikali kupitia hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma lengo likiwa ni kutoa huduma kwa wagonjwa wanaovunjika mifupa.

"Hupatikanaji wa vifaa hivi utatuwezesha kuwahudumia wananchi waliopata ajali kwa haraka zaidi na kwa ufanisi ili wapone ndani ya muda mfupi,"amesema Mganga Mfawidhi.

Naye Daktari bingwa wa mifupa katika hospitali hiyo, Dk Elias Mashala amesema msaada huo ni mkombozi kwao katika utabibu wa mifupa katika mkoa wa Arusha kwani upatikanaji wa vifaa hivyo utasaidia kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

"Vifaa hivi vitatuwezesha sisi kutoa huduma ya mifupa mirefu ya miguu na mikono kwa ufanisi na uhakika zaidi hivyo tunashukuru serikali ya Tanzania kwa kutuletea vifaa hivi katika hospitali yetu,"amesema Dk Mashala.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest amesema wamekabidhi vifaa hivyo kwa lengo la kuhakikisha kila hospitali za mikoa zinazotoa huduma ya mifupa kwa wagonjwa wanaovunjika.

"Lengo ni kuhakikisha wanatoa huduma mfanano katika hospitali zote zinazoanzia ngazi ya mikoa na huduma hii inatolewa kwa watu wa rika zote ,"amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live