Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Mloganzila yapigwa jeki

11a81b9463242a39491f1f9c6067dec0 Hospitali ya Mloganzila yapigwa jeki

Wed, 25 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 45, ambao unalenga kuisaidia hospitali kuendelea kutoa huduma bora.

Msaada huo umetolewa na na taasisi ya Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) kwa kushirikiana na Africa Future Foundation na Jeju National University Hospital na Legbase.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk. Julieth Magandi, ameishukuru taasisi hiyo kwa uhusiano mzuri na Mloganzila na kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma za afya na kusema vifaa hivyo vitasadia utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

“KOFIH ni wadau wetu wakubwa na wanasaidia kuboresha huduma za afya, pia naahidi kuwa msaada huu utaenda kutumika kama ulivyokusudiwa, ili wananchi waendelee kunufaika na huduma bora za afya,” amesema Dk Magandi.

Akikabidhi msaada huo, Mwakilishi wa KOFIH, Sean Hong amesema wanayo furaha kukabidhi msaada huu, ambao utasaidia wataalamu wa afya kufanya kazi zao kwa ufanisi.

"Tutaendelea kutoa msaada kadri watakavyojaliwa, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kama inavyotakiwa,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live